Tuesday, November 24, 2015

FAHAMU NA ZITAMBUE TOFAUTI KATI YA IPHONE ORIGINAL NA CLONE 2

Katika chapisho lililopita tulijifunza jinsi ya kutofautisha iphone fake na original kwa kuiangalia kwa maumbile tuu.
leo tunaenda deep na kujifunza kutofautisha sim hizi mbili kwa kuitumia {perfomance}


  1. Tazama welcome screen zima sim kisha washa na tazama log in screen. Fake nyini huonyesha logo ya Android ama maneno kama welcome, wakati original yenyewe huonyesha logo ya Apple. Pia jaribu kuangalia katika home screen na ufungue app ya AppStore ikikupeleka playstore basi tambua ni fake.
  2. Cheki Application ya Siri Hii ni App ambayo iDevices tuu ndo zina uwezo wa kusoma na kuirun. hivo kama si original itashindwa kabisa.
  3. Tazama Operating Systeam Kama utaona kitu chochote tofauti na iOS basi jua hio sim ni feki kabisaa. iPhone inatumia iOS tuu na si vinginevo
  4. Unganisha kwenye iTunes Unganisha sim yako na kompyuta yako kupitia waya na fungua app ya iTunes kwenye Laptop/Pc yako. kama haitasoma sim ako basi jua tayari ni fake
Asanteni sana na hapa tumefika mwisho wa muendelezo wetu wa jinsi ya kutambua iPhone ya halali na Fake one. Tembelea ukurasa huu mara kwa mara kujionea machapisho mapya. pale ambapo unakwama uliza kwenye comment box au tuandikie barua pepe kupitia techedutanzania@gmail.com
                                              asanteni sanahttps://en.wikipedia.org/wiki/IOS

Sunday, November 22, 2015

FAHAMU NA ZITAMBUE TOFAUTI KATI YA IPHONE ORIGINAL NA CLONE

IPhone ni moja ya gadgets maarufu katika soko. Hii imethibitishwa na mauzo kuongezeka na pia ubora wa bidhaa kua maintained. pia IPhone inazidi kua maarufu kutokana na perfomance na pia heshma anayopata mtumiaji wa sim hii. Apple wameitengeneza iphone ikiambatana na several apps ambazo zitakusaidia on your daily basis. IPhone mpya kawaida gharama karibu $ 699. inaweza kuonekana kidogo ghali, lakini watu wengi huamini kuwa  thamani ya fedha na bidhaa wanayopata vinaendana. Kutokana na hili basi hata wazalishaji wa sim fake kutumia mgongo wa Apple kupitisha bidhaa zao sokoni.

hapa leo utajifunza tofauti kati ya ile fake na original. Wazalishaji wa sim hizi bandia hujitahidi sana kufanya bidhaa yao kua sawa na ile ya halali ili tuu kumchanganya mnunuzi.Ni ngumu kuwazuia wazalishaji hawa kuacha kuingiza bidhaa zao sokoni. Nini kifanyike ni kuelimisha watu ili kupunguza kuongezeka kwa idadi ya wanaotapeliwa. Kwa wale ambao wanataka kununua iPhone kwa mara ya kwanza, huu utakuwa mwongozo mzuri kwa ajili yenu kutofautisha  iPhone kati ya original na cloned. Kama wewe ni mpenzi wa iPhone, bado unaweza kushare chapisho hili pamoja na familia au marafiki , ili nao kujua kutofautisha kati ya iphone fake na original. Ni bora kuanza na sifa za maumbile na kuhusu program na perfomance yatafuta next time.

JINSI YA KUTAMBUA KAMA IPHONE YAKO NI ORIGINAL
  1. Angalia screws.    IPhone original hutumia screw za  pentalobe, wakati clone  anatumia screws kawaida msalaba.Apple amefanya ivo ili iwe rahisi kutofautisha bidhaa zake na za bandia. 
  2. Angalia eneo la button. jinsi nyingine ya kutambua iphone original na fake ni kwa kuangalia mpangilio wa button. katika original button ya kueka silent na za sauti huwa juu upande wa kushoto. Ila fake nyingi huwa upande wa kulia.
  3. Angalia memory capacity Iphone original inakua na fixed memory 16GB, 32GB, 64GB na 128GB. ila fake lazima watumie external memmory ili kuexpand.hivo basi ukiangalia na ukakuta slot ya memory card jua hio ni fake.
Kwa leo naomba tuishie hapo ila next time tutazungumzia kuifahamu kwa kuiwasha na kuangalia other features asanteni.

Thursday, November 19, 2015

KABLA YA KUNUNUA SIM YA SAMSUNG MKONONI KWA MTU FAHAMU HAYA 2

Karibu katika muendelezo wa jarida lililopita linalohusu kugundua na kuweza kutofautisha sim fake.
Chapisho la mwisho tuliongelea Samsung na leo bado tuko nayo samsung.
kama hukubahatika kusoma hapisho lililoita basi lipate hapa http://techedutanzania.blogspot.com/2015/11/kabla-ya-kununua-sim-ya-samsung-mkononi.html .
Chapisho lilopita tulizungumzia kuitambua sim fake kwa kuitazama, leo tunazama deep kidogo na tutatambua kwa perfomance.

TAMBUA CLONED GALAXY KWA KUCHEKI PERFORMANCE

  1. PIGA PICHA NA ANGALIA UBORA WA PICHA ZOTE MBILI {kwa sababu uko na zote mbili itakua rahisi kujua Original ambayo itatoa picha nzuri na fake ambayo itatoa picha mbaya.
  2. CHEZA MAGEMU MAKUBWA YANAYOHITAJI GRAPHICS YA KUTOSHA. GAMES KAMA FIFA 15, D-DAY NA CONTRACT KILLER.
  3. ZIMA NA WASHA DEVICE. FAKE HUWA INACHUKUA MUDA KUZIMA NA KUWAKA
Kwa sasa tuishie hapo ila bado mengi yanakuja
Kwamaswali na mapendekezo tuandikia kwa comment box au barua pepe yetu 
asanteni


Wednesday, November 18, 2015

KABLA YA KUNUNUA SIM YA SAMSUNG MKONONI KWA MTU FAHAMU HAYA

Wengi wetu tumekua tukipenda kununua sim mikononi mwa watu {second hand} kutokana na unafuu wa bei. ila kumekua na ulaghai na utapeli hasa kwa wale wasiojua kutofautisha kati ya sim original na fake. Leo nitazungumzia sana sim za samsung, kwani ndio zimerindima humo mitaani mwetu.
                 Simu za  Samsung Galaxy ni moja ya simu maarufu katika soko. Kila mwaka, kampuni ya samsung hutoa bidhaa mpya ya Galaxy, ambayo kwa kifupi huwa ni bora na muendelezo wa toleo lililopita. Hii ni moja ya sababu inayopelekea wazalishaji wa sim fake {cloned } kutumia mwanya huo kuingiza sim zao sokoni. Tofauti na iphone kwa kutumia iOS programu ya Apple ambao wao pekee ndo licensed owner , Simu za Samsung Galaxy hutumia Google open source ya Android na kuifanya rahisi na nafuu kwa wazalishaji wa clone na feki.
JINSI YA KUTAMBUA GALAXY FAKE NA ORIGINAL
Je umewahi kununua Samsung Galaxy Note 3/4/5 na sasa unahisi ni fake kwa sababu ya performance ndogo? Je? umeona mahali simu ya samsung inauzwa kwa bei rahisi sana ila unaogopa kununua kwa sababu unahisi ni fake? usipate tabu kwani nitakufahamisha kwa undani zaidi jinsi na namna ya kutambua hilo.

TAMBUA SAMSUNG FAKE KWA KUITAZAMA TUU
Simu nyingi za Clone zinakua zimetengenezwa kwa kutumia material za bei rahisi kutokana na bajeti iliokua imepagwa hasa na watu wa masoko. Hivyo kusaidia kuwa rahisi zaidi kufahamika kwa kuitaza tuu. Yafuatayo ni maeneo au mambo muhimu ya kutazama.
NB: kama huna uzoefu na simu original ni bora kuazima ya rafiki ili unapoenda kununua uziweke zote bega kwa bega na kuzilinganisha.


  1. SCREEN IMETENGENEZWA KWA KUTUMIA CHEAP GLASS MATERIAL {kwa kutumia kiganja chako jaribu kurub screen zote mbili na kuskizia tofauti moja huwa rough na ingine smooth}
  2. SCREEN IKO MBALI SANA NA UKINGO {EDGE } ZA SIMU
  3. LOGO YA SAMSUNG HAIJAWA SMOOTHED NA UNAWEZA KABISA KUFEEL PALE UNAPORUB
  4. HOME BUTTON HAIKO KATIKA EXACT POINT INAPOTAKIWA KUWA, HUWA JUU ZAIDI AU CHINI ZAIDI YA ILE YA ORIGINAL
  5. BAADHI YA SENSOR ZINAKUA HAZIPO
  6. SCREEN YA FEKI SI BRIGHT NA SMOOTH KAMA YA ORIGINAL
  7. UKIFUNGUA KWA NYUMA UTAKUTA KUNA VITU VINATOFAUTIANA KWANZIA NATI ZILIZOFUNGIWA MPAKA MAANDISHI NA LOGOZ
  8. USAWA WA SIMU PIA NI TOFAUTI, MOJA HUWA KUBWA NA NYINGINE NDOGO JAPO KWA millimeter CHACHE SANA {ushauri, unapoenda jaribu kubeba cover ambalo linafiti vizuri kwenye sim original.}
  9. KWA SIMU KAMA NOTE 3/4/5 TOA KALAMU {S-PEN} NA JARIBU KUTOFAUTISHA {ya fake hua na point ya metal, ya original huwa na pointer ya ruber. Ya fake kuna features haiwezi fanya kama screen grab na pia screen wright.}
Kwa leo tuishie hapo ila nitakuja tena na chapisho lingine kuhusu simu hizihizi ila sasa kwa kutumia mbinu zingine mbalimbali. kama una swali lolote uliza ama tuandikie kupitia techedutanzania@gmail.com

Monday, November 16, 2015

WASALAM WATANZANIA

Salam kwanu ndugu zangu wa Tanzania, Techedu (Technology Education) ni sehemu ambayo utakua ukipata maelekezo na mafunzo mbalimbali juu ya Technologia hasa katika ulimwengu huu wa digital.
kutakua na Tutorial (Mafunzo) mbalimbali juu ya kutatua matatizo kadhaa.
kwa wenye maswali au mapendekezo, tunathamini sana michango yenu na tunawaomba mtuandikie kupitia techedutanzania@gmail.com.